Baada ya Miaka 11 Kitengo cha kuwafuatilia Waislaam cha Mjini New York chafutwa. waislamu tunajifunza nini?
Polisi hao walikuwa wakitumwa wakiwa wamevalia sare zao za uraiani na kwenda kuwafuatilia mwenendo wa Waislaam na walikuwa wakisikiliza mazungumzo yanayozungumzwa baina ya Waislaam huko wakitumia vifaa vya mawasiliano yenye teknolojia ya kisasa wanapokuwa kwenye migahawa na mahoteli ya kulia vyakula,na pia kwenye Sehemu za Ibada kama Msikitini na za Sokoni.
Kitengo hichi kilichopewa jina la The Demographic Unit hivi karibuni aliteuliwa mwanaume mmoja aitwaye Wiliam J Bartton ametaja kuwa ni kuwa ukiukwaji wa haki za Binaadamu jinsi walivyokuwa wakikusanya siri za Waislaam kwa viongozi waliokuwa kabla yake.
Hata hivyo vitendo hivyo ilikemewa sana na makundi yanayotetea haki za raia ndani ya Marekani inayojulikana kama "Civil Rights" na wameitaja jinsi walivyokuwa wakifanyiwa ujasusi dhidi ya Waislaam imeleta kutoaminiana na hivyo kuweza kuhatarisha usalama wa taifa zima la Marekani.
Polisi hao wa Askari kanzu walikuwa wamejiwekea tabia ya kuwafuatilia Waislaam waonapo Muislaam yeyote imma kwa Mavazi yake au sura yake kuonyesha dalili za Uislaam na kupelekea kumfuatilia maisha yoke yote hata akiingia sehemu za Kinyozi au Mgahawa.
Mradi huo pia ulikuwa ukikusanya taarifa ya Wanafunzi wa Kislaam,Majina yao,namba za simu,na sehemu wanakoishi pamoja na idadi ya watu wanaoishi nao ndani ya majumba zao.
Pia walikuwa wakifuatiliwa Mashekhe waliokuwa wakiwatembelea shuleni na kwenye Vyio vikuu,na wanafunzi wanaohudhuria kwenye mihadhara zao.
Miradi hiyo iliwafanya Waislaam waliokuwa wakifanya kazi ya Polisi mjini New York NYPD kuacha kazi zao huko wakikasirishwa na vitendo hivyo dhidi ya Waislaam na namna walivyokuwa wakifuatiliwa na pia kuwapa kazi za watu waliokuwa wakiwafuatilia kwa namna mmoja au nyingine ya kuwafuatilia waislaam kwenye misikiti na wanafunzi waislaam wanaosoma kwenye Vyio vikuu .
Mwezi October,2012 kijana wa Kislaam Shamiur Rahmaan mwenye asili ya Bangladesh ameikashifu namna walivyokuwa wakiwatumia Polisi wa NYPD kuwapa kazi ya kuwafuatilia Waislaam na kukusanya taarifa za Waislaam ndani ya Misikiti.
Kijana huyo mwanzoni alikamatwa na bangi na baadae Polisi wakamwambia ili tuweze kuufuta kesi yako tuweze kufanya kazi pamoja na ujira wako utakuwa Dola $1000 na marupu rupu ikiwa zaidi kwa mwezi.
Kijana huyo alikuwa akifika Msikitini na alikuwa akianza kuwatolea Waislaam mazungumzo ya Jihadi ili kuweza kuangalie aliye na fikra hiyo,Mwishowe Kijana huyo Allah alimfahamisha na kutubia na kutoa udhuru kwa waislaam na kuongeza kuwa kila aliyemfanyia Ujasusi Polisi hao walikuwa wakimwambia kuwa ni "Mfalani? enh! huyo tunamfahamu hana mapya wala hatari achana nae!".
Sababu kubwa ya kufutwa kitengo hicho ni baada ya Polisi kukiri kuwa baada ya miaka 11 ya ufwatiliaji na ukusanyaji wa taarifa na mazungumzo ya Waislaam hawakuweza kupata taarifa yeyote kuhusiana na maandalizi vitendo vya "Kigaidi".